Headline

Van der Pluijm aaga Yanga kwa ushindi

Yanga wamefanikiwa kumaliza vyema mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwa kuwandika Maafande wa Ruvu Shooting kwa mabao 2-1

Bao la ushindi lililofungwa dakika ya 57 na Nahodha Haruna Niyonzima lilitosha kuipa pointi tatu timu ya Yanga na kumuacha kwa furaha kocha Mdachi Hans van der Pluijm ambaye huo ni mchezo wake wa mwisho kuifundisha timu hiyo.

Ushindi wa leo wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting unaifanya Yanga kumaliza mzunguko wa kwanza ikiwa nafasi ya pili na kujikusanyia pointi 33 alama mbili nyuma ya vinara wanaongoza ligi Simba wenye pointi 35.

Ruvu Shooting ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa na winga wake Abrahaman Mussa dakika ya 6 na kuwapa presha Yanga ambao waliokuwa wamepania kushinda mchezo huo ili kumuongiza gepu la pointi Kati yao na vinara Simba.

Yanga iliyocheza kwa presha kubwa baada ya kufungwa bao hilo, ilijitahidi kupambana kutafuta bao la kusawazisha kupitia kwa washambuliaji wake Simon Msuva, Amissi Tambwe na Donald Ngoma lakini walinzi wa Ruvu waliokuwa makini kuuondosha hatari hizo.

Baada ya kupata bao hilo wachezaji wote wa Ruvu walirudi nyuma na kucheza kwa kujilinda na kuwaacha Yanga wakiutawala mchezo huo kwa kufika mara nyingi kwenye lango la wageni wao lakini papara iliwafanya kupoteza nafasi walizozipata.

Yanga iliendelea kupiga presha kwenye lango la Ruvu Shooting na dakika ya 32 winga Simon Msuva alifanikiwa kuisawazishia timu yake baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Nahodha Niyonzima aliyempiga chenga beki Mao Bofu na kutoa pasi kwa mfungaji.
Kuingilia kwa bao hilo kulionekana kuwarudisha mchezoni Yanga na kuzidi Kupanga mashambulizi lakini wapinzani wao waliokuwa makini kwa kuondosha hatari zote langoni mwao.

Mshambuliaji Issa Kanduru wa Ruvu Shooting,   marakadhaa alionekana kuwasumbua mabeki wa Yanga Kelvin Yondani na Vicent Andrew na wakati mwingine alilazimika kutumia Visio jambo lililosababisha mwamuzi kumuonyesha kadi ya njano.

Mshambuliaji Obrey Chirwa nusura aifungie Yanga bao la pili dakika ya 41 baada ya shuti alilopiga kupabguliwa na kipa wa Ruvu Abdallah Rashid, na mpira kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Amissi Tambwe naye alipata nafasi nzuri dakika ya 43 lakini akashindwa kumaliza pasi nzuri ya Ngoma na mpira kutoka nje na mwamuzi kupuliza filimbi ya mapumziko.

Wakati timu zikienda mapumziko kocha wa Yanga Hans van der Pluijm alimfuata mwamuzi wa mchezo huo na kumlalamikia kuiminya timu yake na kuwapendelea wageni wao Ruvu Shooting ambao walionekana kucheza rafu nyingi huku alipoteza muda kila wakati.

Kipindi cha pili Mwamuzi huyo alimtoa nje kocha Pluijm na kuifanya timu hiyo kucheza kwa maelekezo ya kocha msaidizi Juma Mwambusi.

Yanga waliendelea kucheza kwa nguvu kutafuta bao la ushindi kwa kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la Ruvu  lakini mambo yalikuwa magumu kwao.

Katika dakika ya 57 Nahodha Niyonzima alifunga bao la pili kwa timu yake akipigashuti kali kufuatia shambulizi la kustukiza likianzia kwa Ngoma.

Baada ya kupata bao hilo kuliwazindua Ruvu na kuanza kuliandama lango la Yanga na kufanya mashambulizi kadhaa kwenye lango la Yanga lakini kipa Beno Kakolanya aliyepangua michomo mingi.

Katika dakika ya 79 Mshambuliaji Said Dilunga aliopiga kichwa na mpira kugonga mwamba wa juu na mpira kurudi uwanjani na kuokolewa na walinzi wake.

Simon Msuva wa Yanga naye aliweza kupata nafasi nzuri dakika ya 82 lakini baada ya kufunga alimtoa pasi kwa Tambwe ambaye haikuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga.

Mchezo huo uliendelea kuwa na ushindani huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini Yanga ndio waliopoteza nafasi nyingi za mabao.

No comments