Eshe Buheti: Mabadiliko Hayakwepeki
Anatambulika kwa jina lake halisi la Eshe Buheti. Ni miongoni mwa waigizaji waliotumia majina yao vyema katika tasnia ya filamu nchini.
Buheti alifanya mahojiano na gazeti hili kuhusu masual mbalimbali ikiwamo mtuzamo wake katika tasnia ya filamu, unio wa tamthilia, anavyowazungumzia wakongwe na mabadiliko katika filamu.
Mtazamo wake
Anasema mtizamo wake ni kujipanga na kuja upya hasa baada ya kipindi hiki cha mpito kupita.
Anasema kinachoendelea katika tasnia ya sanaa hakiwezi kuwa hivi lazima wahusika watachukua hatua hivyo wakati muaaka ukisubiriwa wasanii hasa wa filamu wachekeche ubongo na lubuni viti vipya watakaporudi rasmi.
Anafafanua kuwa kukaa na kusubiri mustakabali utakapofima ndiyo kila mmoja aanze maana yake ni kurudi nyima badala ya kusonga mbele, hivyo maandalizi ni sasa na uigizaji ndiyo kazi na lazima kazi iendelee.
Tamthilia
Kuhusu tamthilia Buheti anasema ni mlango mwingine unaofungua njia kwa waigizaji wapya na wakongwe kuchuana kwenye jukwaa moja au majukwaa tofauti lakini kwa lengo moja la kutoa burudani.
Anasema licha ya filamu kulipa kiasi, zilikuwa hazitou fursa kwa waigizaji wa aina zote kuonyesha uwezo wao badala yake ziliwabeba wachache.Anafafanua kuwa ujio wa waigizaji kutoka katia tasnia nyingine za sanaa ikiwamo warembo, wanamitindo na waimbaji kulikimbiza baadhi ya wasanii wa filamu hasa wakongwe, lakini tamthilia inawakusanya wote na kuwapa nafasi ya kujiacjia na kuonyesha uwezo wao.
“Pamoja na yote pia inalipa tofauti na filamu iikuwa ukipata umepata na ukikosa umekosa ndiyo basi”.
Wakongwe
Anasema kama una kipaji hakuna msanii mpya wala mkongwe, cha msingi ni kusoma njia zao wapi walifanikiwa, sababu zipi ziliwakwamisha na walifanya nini ili wafanikiwe baada ya hapo ni kukamua.
Anaeleza umuhimu wa kuwa karibu nao kuwa ni kupata nafasi ya kufahamu mambo mengi zaidi, lakini hicho siyo kikwazo cha mwigizaji mchanga kuogopa kufanya anachoweza kwa kuhofia wakongwe. Kuhusu kuwekwa kando anasema hilo ni kosa ambalo inawezekana ndiyo sababu ya kuwapo kwa filamu za ajabu, zisizo na ubora tasniani.
“ Jungu kuu halikosi ukoko, tunapaswa kuwa nao kwa sababu wanajua vitu vingi ikiwamo namna ya kuwavutia watizamaji na vitu wanavyopenda”.
Usasa
Anasema usasa katika filamu haukwepeki ikiwamo kuchanganya lugha, mavazi, miondoko na hata vitu vinavyoigizwa.
Anafafanua kuwa ni kujidanganya kukwepa mambo hayo kwa sababu dunia ni kijiji na kinachofanyika Tanzania siyo ajabu kuonwa na dunia nzima hivyo mabadiliko ni lazima.
Mchanganyiko wa mataifa
Anazitaja faida za kushirikisha nchi nyingine katika tamthilia kuwa ni kuongeza mashabiki na kujifunza vitu vipya kutoka kwa wengine.
No comments