Headline

Carrera: Chelsea itatwaa ubingwa Uingereza

Carrera ambaye alikuwa msaidizi wa Conte Juventus na Italia amedai kuwa Muitaliano mwenzake huyo anaweza kutwaa ubingwa Uingereza akiwa na Chelsea

Msaidizi wa zamani wa Antonio Conte, Massimo Carrera anaamini Chelsea inaweza kutwaa ubingwa wa ligi huku akielezea maisha yake katika Spartak Moscow.

Kocha huyo wa Spartak alikuwa msaidizi wa Conte akiwa Juventus na Italia kabla ya kutimkia Urusi wakati Conte akielekea Uingereza.

“Antonio ni moja ya makocha bora duniani, na kwangu mimi ilikuwa kama kupata mafunzo ya muda mfupi,” Carrera alikiambia La Stampa.

“Ilikuwa safi kwenye kufundisha miaka michache katika Serie B au C, anaweza kushinda Ligi Kuu Uingereza, tuliongea Jumamosi.”

Carrera alitimkia Urusi kama kocha msaidizi katika Ligi Kuu, lakini punde akawa kocha mkuu.
“Waliniita baada ya Euro. Nilikuwa na imani kwamba ningeenda Chelsea pamoja na Conte, na nilipenda sana wazo hili, lakini mambo yakawa tofauti.

“Agosti baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Europa hatua za awali na kujiuzulu kwa [Dimitri] Alenichev, waliniomba: ‘unajisikia kuongoza benchi kwa mechi mbili?’.

“Nilijaribu, bila kufikiri sana juu ya mustakabali. Baada ya michezo 12 tulikuwa juu, na pointi tatu zaidi ya timu ya pili na saba zaidi ya timu inayoshika nafasi ya tatu.

“Ni vema kucheza nyumbani? Siyo mara zote. Daima huwa tunafanya mazoezi katika uwanja wa mazoezi wa Spartak ambako naishi km 40 kutoka Moscow. Mahali ambapo ni pazuri licha ya jambo moja: Foleni.

“Kuhusu vyombo vya habari? Safi! Naweza kuelewa wanachoandika! Lakini nadhani nitalazimika kusoma Kirusi.

“Kwa sasa naongea Kiitaliano, na mtafsiri wangu hutafsiri kwenda Kirusi. Nina bahati kuwa na [Salvatore] Bocchetti ambaye ameishi Urusi kwa miaka mingi.

“Lugha za mpira wakati mwingine ni rahisi kwani tunazungumza kwa vitendo.
“Vodka? Vinywaji vya pombe vyote vimezuiliwa kwenye uwanja wa mazoezi, Natumai itakuwa hivyo hata nyumbani…”

No comments