Headline

SIMBA WANATAKA FEDHA KUMRUHUSU KESSY KUCHEZA YANGA

Simba wanataka Yanga iwapatie fedha ili waandike barua itakayomuidhinisha Hassan 'Kessy' Ramadhani kucheza katika michuano ya Shirikisho CAF
Kessy
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema, lazima Yanga wawapatie kiasi cha pesa ili waweze kuandika barua ya kumtumia mchezaji Hassan Ramadhani ‘Kessy’ kwenye michezo ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Hans Poppe amesema, wanafanya hivyo kwa sababu kipindi cha kuidhinisha usajili kwa Tanzania Bara hakijawadia, hivyo ili Yanga waweze kumtumia ni lazima kuwepo barua ya kumruhusu kutoka kwa Sismba timu ambayo aliichezea mara ya mwisho.
“Tunasubiri pesa kutoka kwa Yanga, ili tuweze kuandika barua ya kumruhusu Kessy, kucheza mechi zao za kombe la Shirikisho vinginevyo hatuta mruhusu hadi hapo usajili utakapopitishwa,” amesema Hans Poppe.
Yanga iliamua kutomtumia Kessy na wachezaji wengine watatu iliyowasajili kwenye dirisha dogo la usajili wa CAF, kwenye mchezo huo wa Jumapili usiku kutokana na kutokuwa na barua kutoka kwenye timu walizokuwa wakichezea awali ingawa CAF, ilishatoa leseni zao.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusidedit amesema hawatotoa kiasi chochote cha pesa kwa uongozi wa Simba na kama watashindwa kuandika barua hiyo watasubiri hadi hapo usajili wa Tanzania utakapoidhinishwa.

chanzo;-
Goal.com

No comments