Headline

NIKI WA PILI; ''TUNAJIFUNZA SANAA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII''

Msanii Niki wa Pili kutoka katika kundi la Weusi amefunguka na kusema wasanii wengi nchini wanajifunza sanaa magetoni, mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kama You tube ambako kote huko hakuna maadili ya sanaa kama ilivyo katika fani zingine ambazo  watu huingia radasani na kusomea fani hizo ambazo mwisho wa siku zinakuwa na misingi ambayo watu wa kada hizo wanapaswa kuzifuata.

Nikk wa Pili aliandika haya kupitia ukurasa wake wa Instgram na kusema inapaswa sanaa nchini ifundishwe darasani kuanzia chekechea mpaka form six kwa kuwa na mitaala katika shule za Umma, tofauti na hali ilivyo sasa ambapo sanaa inaanza kufundishwa chuo.

“Nakumbuka zile takwimu za BASATA zinazo sema Tanzania inakadiriwa kuwa na wasanii milioni 10. Lakini mbona sanaa siioni katika mitaala ya elimu ya umma kuanzia chekechea mpaka form 6. Lakini kuna chuo cha Bagamoyo na Mlimani kuna kitivo cha sanaa sasa hii si ajabu unaanzaje kujifunzia sanaa chuo jamani? alihoji Nikk wa Pili
Nikk wa Pili amezidi kuwaomba viongozi mbalimbali waweze kuangalia mfumo wa elimu nchini ili uweze kuitambua sanaa kwani kwa kufanya hivyo wasanii watakuwa na maadili kwa kuwa watajifunza somo la maadili ya sanaa kama ilivyo kwa watu wanaojifunza fani zingine ambao hujifunza maadili ya kazi zao.
“Waeshimiwa wote mliopigiwa kampeni na wasanii, hebu jiulizeni hivi hasa wasanii katika mfumo wenu wa elimu, wao wako wapi. siyo tu kusema wasanii wanatutangaza kimataifa, wakati mfumo wenyewe wa elimu wa kitaifa hauitambui sanaa. Ama kusema wasanii hawana maadili, sanaa tunajifunzia magetoni, mitaani, youtube huko kote hamna maadili. Tungejifunzia darasani huenda kungekuwa na somo la sanaa na maadili. kama tu unavyo jifunza Procurement Ethics…..au maadili ya udaktari” aliandika Nikk wa Pili

No comments