Headline

KIBARUA CHA MKENYA TOM OLABA KIMEOTA NYASI

Timu ya Ruvu Shooting imevunja mkataba na kocha wake mkuu Mkenya Tom Alex Olaba na nafasi yake wamempa aliyekuwa msaidizi wake Seleman Mtungwe mwenye leseni B inayoruhusiwa kufundisha timu ya Ligi Kuu.Msemaji wa timu hiyo Masau Bwire amesema, wanamshukuru Olaba kwa kazi yake nzuri tangu alipojiunga nao 2014 kuchukua nafasi ya Boniface Mkwasa,aliyekwenda kujiunga na Yanga.
Wakati Olaba anaanza kuifundisha Ruvu Shooting msimu huo wa mwaka 2014/15 aliikuta ikiwa na point 17, mpaka mwisho wa ligi Ruvu Shooting chini ya Olaba ilimaliza ikiwa nafasi ya 5, point 35.
Msimu wa 2015/16 Ruvu Shooting chini ya mwalimu Olaba haikufanya vizuri kwani ilishuka Daraja ikiwa na jumla ya pointi 29 japo kushuka kwake inasemakana kulitokana na hujuma nyingi hasa katika mchezo wa mwisho wa msimu huo wa ligi ikicheza ugenini na mwenyeji Stand United kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga!
Olaba pamoja na kushuka kwa Ruvu Shooting, alikubali kushuka nayo hadi ligi Daraja la Kwanza akiahidi kuipandisha daraja, ahadi ambayo aliitekeleza.
Katika ligi hiyo ya FDL tulicheza kwa mafanikio makubwa tukiwa kundi B nakufanikiwa kumaliza nafasi ya kwanza na kurejea Ligi ya Vodacom msimu ujao  chini yake
"Ruvu Shooting tunaheshimu sana mchango wa Olaba katika timu yetu na tunamheshimu sana Olaba, tutaendelea kumheshimu na kuamini kuwa ni miongoni mwa makocha bora katika ukanda huu wa nchi za maziwa makuu na Afrika,"amesema Bwire.

No comments