ZLATAN IBRAHIMOVIC KUSTAFU TIMU YA TAIFA
Mkongwe huyo wa miaka 34 atatundika rasmi daluga zake rasmi kuichezea Sweden michuano ya Euro 2016 itakapomalizika na tayari ameshaanza kuwashukuru mashabiki
Zlatan Ibrahimovic |
Zlatan Ibrahimovic ametangaza kuwa atastaafu soka la kimataifa baada ya Euro 2016.
Sweden watashuka dimbani kuikabili Ubelgiji Jumatano ambayo inaweza kuwa mechi ya mwisho kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa PSG kwa nchi yake, Sweden kwa sasa wana pointi moja tu, 2 nyuma ya wapinzani wao wanaoshikilia nafasi ya pili kwenye kundi.
Akizungumza na vyombo vya habari kuelekea mchezo wao huo, Ibrahimovic alisema: "Mechi ya mwisho ya Sweden kwenye michuano ya Euro itakuwa ndiyo mechi yangu ya mwisho kwa nchi yangu. Sitashiriki kwenye michuano ya Olimpiki.
"Hivyo mechi yangu ya mwisho ya Euro itakuwa ndiyo ya mwisho. Tuombe kudumu kwenye michuano hii kwa muda. Natumai mechi ya kesho haitakuwa mechi yangu ya mwisho, lakini sina majuto yoyote.

"Sijavunjika moyo kwa lolote. Najivunia kuwa nahodha wa Sweden.
"Nataka kutumia fursa hii kuwashukuru mashabiki wote kwa ushirikiano wao kila nilipokuwa, daima nitaibeba bendera ya Sweden na kusimama nayo imara."
No comments