TINO ALIA NA FILAMU ZA NJ'EE
NYOTA wa filamu Hisany Muya ‘Tino’ anasema kuwa sinema kutoka nje zimeua soko la ndani na kuwafanya wasanii waishi kwa shida kwani hata watengeneze kazi zenye ubora wa namna gani bado wanashindwa kuuza kwa bei ya kimaslahi.
Hisany Muya ‘Tino’
“Serikali tunaomba itusaidie kwa hili sinema kutoka nje ni tatizo ndio zimeua soko letu, hazilipi ushuru zimezagaa kila kona huku zikiuzwa kwa bei ya kutupwa kwa hiyo bora sisi tufe njaa Wachina wanemeke,”anasema Tino.
Toka urasimishaji wa filamu na muziki hali imekuwa mbaya sana kwa wasanii wa filamu kwani soko la filamu kutoka nje limeshika hatamu huku tamthilia za kifilipino zilizotafsiriwa zikitamba mitaa yote ya Kariakoo na kuzifunika kazi za ndani ambao ndio walipa kodi.
No comments