SIMBA SC YAKARIBIA KUMNASA KOCHA KUTOKA GHANA
Klabu ya Simba inakaribia kuinasa saini ya kocha maarufu Afrika Sellas Tetteh Teivi, raia wa Ghana kutokana na mazungumzo kwenda vizuri
Zacharia Hans Poppe amesema wamefanya mazungumzo ya awali na wameona kunamwelekea mzuri wa kumnasa kocha huyo ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya taifa ya Sierra Leone.
“Tumefanya naye mazungumzo kwa wiki moja na mambo yanaelekea kuwa sawa pengine tukamtangaza kabla ya kumaliza zoezi la usajili na yeye akatusaidia kufanya usajili wa kikosi chetu cha msimu ujao,”amesema Hans Poppe.
Kocha huyo aliyewahi kuinoa timu ya taifa ya Ghana, ni maarufu kutokana na mambo kadhaa likiwemo lile la kuiongoza timu ya vijana wa Ghana chini ya miaka 23 kucheza Kombe la Dunia mwaka 2013.
No comments