Headline

RASMI TELELA ATEMWA TANGA TINOCCO ATOLEWA KWA MKOPO

Yanga imeweka wazi mpango wake wa kuachana na wachezaji wawili kwenye kikosi chao cha msimu ujao ambao ni kiungo Salumu Telela na kipa Benedictor Tinocco ambaye atatolewa kwa mkopo kutokana na kuwa na mkataba mrefu na timu hiyo.
Eliya95  imezipata taarifa  kutoka kwenye klabu ya  Yanga  kwamba maamuzi hayo yamepitishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm.
“Tinocco atatolewa kwa mkopo sehemu ambayo anaweza kupata nafasi ya kucheza, ili kama atapandisha uwezo wake, anaweza kurudishwa, lakini Telela kocha (Pluijm)” kimesema chanzo kutoka Yanga.
Bado haijafahamika haswa sababu za Telela kutoongezewa Mkataba, licha ya umuhimu wake wa wazi unaoonekana katika timu kwa sababu ni kiraka anayeweza kucheza kama beki wa kulia, kati na nafasi zote za kiungo.

Na kuhusu suala la nidhamu, Telela anaonekana ni mchezaji mwenye nidhamu, bidii ya mazoezi na kujituma, ambaye wakati wote anapoingizwa uwanjani licha ya muda mwingi kuwa mchezaji wa akiba hucheza vizuri. 
Wakati huo huo, Yanga inaendelea kusubiri ofa ya kumuuza mshambuliaji Paul Nonga ambaye ameombwa mwenyewe kuuzwa, ili kwenda timu ambayo atakuwa anacheza.
Nonga aliyesajiliwa Desemba kwa dau la Sh. Milioni 20 kutoka Mwadui FC ya Shinyanga ameamua kuondoka baada ya kushindwa ushindani wa namba.
Washambuliaji chaguo la kwanza wa Yanga ni Mzimbabwe Donald Ngoma na Mrundi, Amissi Tambwe wakati Nonga alikuwa wa akiba pamoja na Malimi Busungu na Matheo Anthony.  
Tayari Yanga SC imekwishamuacha kiungo kutoka Niger, Issoufou Boubacar ambaye pia alisajiliwa dirisha dogo Desemba.


Telela aliye achwa na timu ya yanga ambayo kwa sasa ipo uturuki kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

No comments