Headline

NAKATA NI SOMO TOSHA

mwandishi@Rajab Mnakane

Mazingatio mema kwa wale wanaojifunza ni kufuata mafundisho mema,Vijana wanaopenda mafanikio yaliyo na mpangilio hujifunza mazuri kutoka kwa waliowatangulia, ama kupitia mazingira yaliyowazunguka. Kutoka kwenye chimbuko la historia ya Hidetoshi Nakata katika soka kuna mazingatio kwa wenye macho na masikio.

 Hidetoshi Nakata alizaliwa tarehe 22/01/1977 pale Yomanashi-Japan na alianza kucheza soka akiwa na umri mdogo katika kipindi cha mwaka 1986 kwenye klabu za mitaani kabla hajachanua 1995.
Katika kipindi hiko Nakata alianza kung'aa katika kiwango cha juu cha soka mpaka mwaka 1997/98 alipotwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa bara la Asia, na akashinda ubingwa wa eskudeto akiwa na Roma 2001 kwenye ligi ya seria A. Nakata ameiwakilisha Japan kwenye michuano ya kombe la Dunia mara 3, ikiwa ni mwaka 1998, 2002 na 2006 huku kwenye michuano ya Olimpiki mara 2, 1996 na 2000.


Mchezaji huyo aliyeng'aa katika eneo la kiungo, alipita katika vilabu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Bellmere Hirats 1995-98, Peragia 1998-2000, Roma 2000-01, Parma 2001-04, Bolognia kwa mkopo 2004, Fiorentina 2004-05 na Borton Wonderous 2005-06.
 Hidetosho Nakata alitangaza kutandika daluga mnamo tarehe 3/07/2006 akiwa na umri wa miaka 29 tu, kutokana na majeraha mara kwa mara baada ya kudumu katika soka kwa miaka 10, ikiwa 7 kwenye seria A kule Italy, 1 kwenye ligi ya Uingereza na 2 kwenye ligi ya Japan.

Gwiji wa zamani katika soka Pele, amemtaja Nakata kwenye listi ya wanasoka bora 100 wa FIFA, wa muda wote na kumfanya kuwa mchezaji pekee kutoka Japan kuingia kwenye listi hiyo, na ni miongoni mwa wachezaji wawili tu kutoka barani Asia, huku mwingine kwenye listi hiyo ni beki wa zamani wa Korea Hong Myung Bo.

No comments