MWENENDO WA KAZI ZA V-MONEY
Juu ya mwendo wa kazi zake, muimbaji wa Tanzania,
mtunzi wa nyimbo, na mwanamuziki nyota Vanessa ametoa nyimbo tano ikiwa ni
pamoja na Closer, Hawajui, Come Over, Wave Clap dance na Siri, pia
ameshirikishwa katika nyimbo kama Me and you na Ommy Dimples, Money na AY,
Monifere na Gosy B, Bashasha na Bob Junior na Nisamehe na Angle.
Vanessa alishinda tuzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na
tuzo nne za Kill Music Awards na moja ya Afrika all Music Award.
Amekuwa akijihusisha na kampeni mbalimbali kama vile
Staying Alive Foundation Project, kampeni ya Zinduka, MTV Africa Music Awards,
Sauti Za Busara, UNAIDS Mkutano wa vijana Mali uliofanyika Bamako, Mkutano wa
Kimataifa juu ya VVU na magonjwa ya zinaa ulofanyika Addis Ababa, Ethiopia.
Mdee amekuwa akiendesha vipindi kama MTV Base meets,
shoo inayolenga kuwawezesha vijana Waafrika kutoka duniani kote kwa kuwapa
fursa ya kukaa chini na kiongozi mashuhuri, Kili Music Awards, Epiq Bongo Star
Search (EBSS), Dume Challenge, 'Switch On' kampeni ya Airtel, Coke Studio
Afrika, Kili Music Tour, Serengeti Fiesta Music Tour, Coca Cola Chart Express,
The Hit ya Choice FM, pan-African TV show na MTV Base select 10.
Alishawahi kupata tuzo katika Gala mjini New York
kutoka kwa UNA-YP, alituzwa na GAVI Alliance kwa msaada wake katika uanzishwaji
wa chanjo bure kwa watoto wa Tanzania. Mdee balozi wa GAVI na mpambanaji dhidi
ya kansa ya kizazi.
Mwaka 2014
alipata mkataba kutoka kampuni ya Crown Paints, kuwa balozi wake nchini
Tanzania.
No comments