MTEGO KUHUSU MICHUANO YA EURO 2016
Mwandishi@Rajab Mnakane
UEFA-EURO rasmi imeanza kutimua vumbi kwa mchezo wa ufunguzi 2016 kwa mwenyeji Ufaransa kuitungua Romania mabao 2-1.
UEFA-EURO rasmi imeanza kutimua vumbi kwa mchezo wa ufunguzi 2016 kwa mwenyeji Ufaransa kuitungua Romania mabao 2-1.
Wakati wapenzi wa
soka wakifuatilia kile kilichotokea kwenye mchezo wa ufunguzi, na kuwaacha
wapenzi wa Ufaransa na raia wake wakifurahia huku Romania na hata wasioipenda
Ufaransa wakihuzunika kutokana na matokeo hayo, nachukua kalamu yangu
iliyotukuka na akili aliyonibaliki Mola mlezi wangu kukukumbusha baadhi ya
rekodi zilizowekwa kwenye michuano hii inayoandaliwa na UEFA kwenye Nchi tofauti
zilizoshiriki kuandaa michuano hii.
Kwa kuwa lengo
langu ni kutaka kukuacha na swali hasa kwa wewe ambaye unabashiri, leo
tuangalie rekodi moja tu iliyowekwa kwenye mashindano haya kuanzia mwaka 2000,
siyo nyingine nayo ni goli la kwanza kuwahi kufungwa katika mchezo wa fainali
kuanzia kipindi hicho. Kumbukumbu zinaniambia mchezo wa fainali ya mwaka 2000
ya UEFA-EURO uliwakutanisha Ufaransa na Italy,...!
mechia ambayo Ufaransa
alishinda 2-1 ila bao la kwanza lilifungwa na Marco Delvecchio dakika ya 55
ambalo lilikuwa la kuongoza kwa Italy wakati sheria ya gorden goal inatumika.
Mwaka 2004 wakati
mashindano hayo yalipoandaliwa kwa mara ya kwanza pale Ureno, wenyeji Ureno
ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa kipindi kile, walikutana na Ugiriki
fainali kwenye uwanja wa Stade de Luz pale Lisbon. Ureno walilala bao 1-0 na
kuwa bao la kwanza na la mwisho kwenye fainali hiyo lililofungwa na Angelos
Charesteas.
Autralia hawakuwa
nyuma kwani nao walipata nafasi ya kuandaa michuano hiyo mwaka 2008 japo wao
hawakupata nafasi ya kufika fainali kama ilivyokuwa kwa Ureno nyumbani. Fainali
ya safari hii iliwahusu Hispania na Ujeruman. Goli pekee lililofungwa na
Ferdnand Torres dakika ya 33, lilitosha kuizamisha Ujeruman na kutengeneza goli
moja tu, yaani la kwanza na la mwisho kwenye mchezo huo ambao ulifanyika Estade Vienna.
Michuano ya mwaka 2012 ambayo Ukraine walishiriki kuandaa mchezo wa fainali
kati ya Hispania tena na Italy kule katika Jiji la Kiev, Hispania ilimfunga
Italy magoli 4-0 ila goli la kwanza kwenye mchezo ule lilifungwa na David Silva
dakika ya 13 akipokea pasi ya mwisho kutoka kwa Fransisc Fabregas Sisc.
No comments