Headline

HADITHI TAMU YENYE KUVUTIA,IMEPELEKEA KUWEPO KWA REKODI LUKUKI DUNIANI

mwandishi@Rajab Mnakane

Michuano ya Copa America ambayo Ikiwa imetimiza mikaka 100 tangu kuanzishwa mwaka 1916, michuano inayoshirikisha Nchi kutoka Amerika ya kaskazini, kusini na visiwa vilivyopo katikati ya mabara ya America Kaskazini na Kusini, kwa mara ya kwanza michuano hiyo inafanyika katika aridhi ya Marekani.

Michuano hiyo ambayo chikumbuko lake ni Mabara yanayotoa wenye vipaji vya asili wenye uwezo wa kucheza mpira mwingi huku wakitumia nguvu kidogo ina hadithi tamu na ya kuvutia ambayo imepelekea kuwekwa kwa rekodi mbalimbali Ulimwenguni.

Wakati Brazil wakishiriki michuano ya kombe la dunia mara 20, Uruguay linabaki kuwa Taifa pekee lililoshiriki michuano ya Copa America mara nyingi likiwa limefanya hivyo mara 40.

 Kama hiyo haitoshi Uruguay hao hao wamechukua kikombe cha Copa America mara nyingi, wakibeba mara 15, huku Argentina ndiyo Taifa lililofika fainali mara nyingi, likicheza jumla ya fainali 26.
Michuano ya Copa America ambayo imejiwekea historia ya kuvutia hapa ulimwenguni, imeishuhudia Uruguay ikiweka rekodi nyingine kwa kuwa ndiyo Taifa lilocheza michezo mingi, likicheza jumla ya michezo 184.
Japan na Jamaica ndiyo Nchi zilizocheza michezo michache, wakati Argentina imeshinda michezo 111 na kulifanya Taifa lilishinda michezo mingi, huku Chile ndio Taifa lilipoteza michezo mingi, likifungwa mara 81.

Argentina na Peru zimelazimishwa sare mara nyingi, zikifanya hivyo mara 31 kila mmoja, huku Argentina linaongoza kwa kufunga jumla ya magoli 422 na Ecuador wameruhusu magoli 296.

 Hii ndiyo michuano ya Copa America ambayo imeyaacha Mataifa ya Uruguay, Argentina na Brazil yakimaliza nne bora mara nyingi.

No comments